Elimu nchini Sudan

Elimu imeimarika kwa kiwango kikubwa kwa miaka 15 iliopita. Haswa wanawake
wamefaidika kiwango kikubwa kwa mpango wa serikali wa maendeleo ya nguvu kazi.

Wasichana ndiyo wanaonawiri hivi sasa kielimu kuliko wavulana, na kwa miaka ijayo
watatawala nyanja za utaalamu zote. Tayari wanawake wako asili mia 70 ya wafanyikazi
wa sekta ya afya, ingawaje wengi ni wauguzi, wenye shahada ya kwanza ya sayansi kutoka
vyuo vya uuguzi. Wizara ya elimu ya juu ilifanya takwimu ya mwezi wa Novemba mwaka
2001 iliyo onyesha kuwa wanawake watakua wengi kwenye kikundi kinacho hitimu hivi
karibuni toka vyuo vikuu.
Repoti hiyo imetoa asilimia ya wanawake katika vitengo tofauti kama vile:
• Tiba na Nyanja zinazo husika 75%
• Elimu 72%
• Vitengo vya kibinadamu 64%
• Kilimo 60%
• Elimu jamii 58%
• Sayansi 51%
• Huduma (Kanuni,uhasibu, utaalamu wa tarakilishi, uhandisi .. na nyinginezo 50%