Kilimo na Ufugaji Sudan

Mazao ya kilimo katika mwaka 1993 -mwaka wa Mpango Mzima wa kitaifa-
yameongezeka kwa asili mia 29 zaidi ya mwaka ulotangulia , kutoka hapo
sekta hiyo ikaanza kua thabiti ikikua kwa kadri ya 5% kwa mwaka mpaka
mwaka wa 1996.
Na kati ya mwaka wa 1997 na 2000 sekta hii inayoongoza
ilikua kwa asili mia 29.9 kwa wastani wa asili mia ya 7.5 . Ufugaji unashikilia
khumusi mbili za thamani ya mazao ya kilimo inayofikia vichwa millioni 140
vya wanyama, Sudan yalenga kuwa msambazaji mkuu wa nyama nyekundu
kupeleka katika nchi za ulimwengu wa kiarabu na kwengineko.

Na huduma za tiba ya wanyama imewezesha kukuwa kwa sekta ya wanyama
mara nne zaidi ikilinganishwa na miaka 40 iliopita. Uzalishaji wa mifugo
imekua ni unatokana na mifugo ya jamii ya kuhamahama, na changamoto za
kupata malisho zimepelekea kupanuka kwa jangwa na kuongezeka kwa mifugo
huku ikiangazia haja ya kutumika kwa mitindo ya kisasa ya uzalishaji wanyama,
ambapo mangonjwa mengi ya wanyama yamewezwa kuthibitiwa na aina ya
wanyama kuimiarishwa, lakini pamoja na hayo , sekta ya ufugaji bado inakumbwa
na kasoro kwenye viwango vya kimataifa, Malisho ya kawaida yana matokeo bora
zaidi kwa nyama ya ng’ombe wa kisudani, kondoo na mbuzi kwani wanakua na
kiwango cha chini zaidi cha mafuta (Cholesterol) jambo ambalo ni kivutio katika
soko la ulimwengu, na hilo laonyesha kuwa njia pekee yakuweza kuboresha namna
ya kuzalisha mifugo ya sudan inategemea kwa ukubwa kuingiza ubunifu kwenye
matumizi ya njia za kijadi za uzalishaji, ambapo jamii za ufugaji zachanganya baina
ya njia hizo walizozizoea za kijadi huku wakiongeza mahitaji ya kuboresha mazao na
namna ya kuishi.