Sekta ya Afya Sudan

Gharama ya huduma za kiafya zimepungua sana, yote hayo ni kwa ajili ya kuepo bima
ya afya inayogharimu Dinari
za kisudani 200 kila mwezi kwa mtu mmoja (kiwango cha
chini ya Dola moja ya kimarekani) na inatoa mapunguzo ya asili mia 75 ya matibabu
katika hospitali za umma, na kupunguza bei za madawa kwenye maduka ya dawa ya
umma, Maduka ya dawa yamesambaa kote yawe ya umma ama ya kibinafsi. Wizara ya
afya inakadiria kuwepo duka la dawa la umma kwa kila watu 1,000, na zihudumu kwa
zamu kuwezesha wanaoishi mbali kuweza kupata dawa kwa wakati wowote iwe usiku
au mchana. Chanjo kwa watoto walo chini ya umri wa miaka 12 yapatikana kote jijini
Khartoum. Maeneo ya mijini yana takriban nusu ya madaktari wote walioko nchini
(takriban 2,500) ingawaje maeneo haya yanabeba chini ya asili mia 20 ya idadi ya watu
wote.

Zaidi ya wanafunzi 1,000 walikua wakijiunga na vyuo vikuu kila mwaka kusomea tiba tangu
mwaka wa 1994. Kuna hospitali ya kujifunza na kituo cha utafiti cha teknolojiya ya miyale ya
lesa kwenye chuo kikuu cha Khartoum. Operesheni nyingi za upasuaji siku hizi zafanywa kwa
lesa wala sio nyembe na visu. Hatua muhimu zimepigwa kwenye sekta ya afya kwa mda unaozidi
miaka 10 iliopita. Kuna muongezeko wa idadi ya hospitali , vituo vya matibabu, wahudumu na
vifaa nchi nzima illa uongezeko huo haupo kwenya maeneo yanayothibitiwa na waasi.