Vyanzo vya maji Sudan

Vyanzo vya maji nchini Sudan ni mvua, mito na maji ya ardhini. Sehemu ya
kusini na ya kati zinapata mvua nyingi kwa mwaka ingawaje maeneo ya kaskazi
ni kame na yana maji mengi ya ardhini.
Kwa mujibu wa mkataba baina ya nchi
zenye vyanzo vya Mto Nile uliyo tiwa sahihi mwaka wa 1959, fungu la Sudan
tokamana na maji ya mto huo ni ‘cubic meter’ billioni 18.5, na matumizi yake
sasa ni takriban ‘cubic meter’ billioni 12.2.

Jumla ya maji yanayo tiririka ni takriban ‘cubic meter’ billioni 3.3. Maji yanayotokea
sehemu za mainuko yanaweza kuhifadhiwa kwenye mahifadhiyo na kwenye machimbo
ilikukidhi mahitaji ya wanadamu na wanyama wa nyumbani. Maeneo ya chini yenye
unyevu na mabirika yamekua tangu jadi kama vyanzo vya maji kwa wanyama na matumizi
ya nyumbani. Na vyanzo vya maji ya ardhini yakadiriwa kufikia trillioni 15.2 ‘cubic meter’
yapatikana ikiwa ni chini ya asili mia 50 ya ardhi nzima ya Sudani. Akiba hiyo ya mda mrefu
ni zaidi ya maji yanayo tiririka kutoka kwa mto Nile ya mwaka mzima kwa mara 200, juhudi
zaendelea ilikueza kutumia akiba ya maji yalioko ardhini ilikupunguza athari ya ukosefu wa
maji ambayo ni hofu kuu ya serikali.